Monday, March 13, 2017

MAISHA:Je unataka kuishi miaka mingi?Hii ni siri saba za kuishi miaka 100 na zaidi

Tokeo la picha la long LIFE



Kuishi karne moja au zaidi duniani ni mafanikio makubwa katika maisha ya binadamu lakini kutokana na kuongezeka sababu zinazopelekea mtu kufa mapema ikiwemo hali ngumu ya maisha na kukosa furaha na amani, imeelezwa kuwa ili uishi muda mrefu ni lazima ufanikiwe katika afya.
Wapo watu waliowahi kuishi miaka 100 na zaidi na wengine wapo hata sasa huku wengi wakiwa na siri za kuishi muda mrefu kiasi hicho.
Mtandao wa indiatime.com kwa msaada wa watu walioishi kwa miaka mingi duniani umezitaja siri 7 ambazo zikizingatiwa zinaweza kumfanya mtu akaishi kwa muda mrefu zaidi.
1: Kutembea sana kwa miguu
George Boggess hakufikisha miaka 105 lakini aliishi zaidi ya miaka 100 aliwahi kutoa ushauri na siri ya kuishi umri mrefu kuwa ni kutembea.

2: Kula samaki na kulala kwa angalau saa 8
Misao Okawa, ambaye alitambulika kama binadamu mkwenye umri mkubwa zaidi dunia ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 117 alisema sushi (samaki) na saa 8 za kulala ni siri ya kuishi kwa muda mrefu.
Wajapan wanatajwa kuwa na uwiano wa kuishi muda mrefu mbapo kuna zaidi ya watu 5,000 wanaosemwa kuishi zaidi ya mika 100.

3: Kupiga push-ups tano hadi saba kila siku
Duranord Veillalord ambaye alitimiza miaka 109 mwaka jana anaianza siku yake kwa pushups kila siku. Pushups, kikombe cha chai na matunda ni siri ya kuishi kwa miaka mingi.

4: Kaa mbali na vipodozi
Adelina Domingues alikuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuishi Marekani ambapo alifariki akiwa na umri wa miaka 114 anasema siri kubwa ya yeye kuishi miaka mingi ni kujiweka mbali na vipodozi.

5: Kunywa uji wakati wa kufungua kinywa
Jesse Gallan aliishi kwa miaka 109 na kusema siri kubwa ilikuwa kunywa uji kama kifungua kinywa chake pia alisema kutokuwa na wanaume wengi kwenye maisha yake kuliongeza miaka ya maisha yake.

6: Kaa mbali na pombe/ulevi
Alexander Imich wa New York City ambaye aliishi kwa miaka 111 alisema siri kubwa ya yeye kuishi miaka 111 ni kwa sababu alijiweka mbali na kilevi na alikuwa muogeleaji na kufanya mazoezi. Chakula chake kilikuwa ni kuku na samaki na kuishi maisha ya kuzingatia kanuni za kiafya.

7: Kula kwa kiasi
Wanawake wa jamii ya Hunza inayopatikana katika mipaka ya Kashmir, China na Afghanistan hupata watoto wakiwa na miaka 60 na wanaume wanaoonekana kama wana miaka 40. Wazee wa jamii hii wamefikisha umri wa miaka mia moja na wangali na muonekano kana kwamba wana miaka 70 ambapo wanajamii hiyo wakisema siri ni kula kwa kiasi. Wanakula nyama kidogo katika milo miwili kwa siku.

Saturday, March 11, 2017

AFYA:Fahamu njia rahisi za kukabiliana na msongo wa mawazo (Stress)

Tokeo la picha la STRESS FREE

Msongo wa mawazo ama stress kwa kiingereza, ni tatizo ambalo kwa bahati mbaya sana limeendelea kuwa kitu cha kawaida sana kwa wanaadamu katika zama tulizo nazo. Katika miaka hii tuliyo nayo, ni sahihi kabisa kusema kuwa, takriban wanaadamu wote walio hai wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hili.
 
Kuna baadhi ya aina za msongo wa kimawazo, ambazo zinaepukika na nyingine ni ngumu kuziepuka ila unapaswa kujua jinsi ya kukabiliana na shinikizo la msongo wa mawazo pale linapokukabili.
 na hali hii pindi unapojikuta umetumbukia ndani yake

1. Jifunze kusema “hapana” hii ni katika mambo yako binafsi au kazi yako, unaitumiaje hii hapana? Unajua maofisini kuna swala la kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, yaani hujamaliza hili unaletea jingine hata kama sio kazi yako… sasa jifunze kukataa hizi kazi zisizo za kwako ili mradi tu mfurahishe tu. hivyo hivyo vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyokuletea msongo wa mawazo.
 
2.Jiepushe na watu ambao mara nyingi wanakusababishia Stress: Unajua ukikaa chini na kufikiria utagundua kuna mtu flani au kundi flani la watu ndo linalokuleta msongo wa mawazo, sasa kaa nao mbali kabisa.
 
3.Simamia mazingira yanayokuzunguka:Mazingira yanakuzunguka yanaweza kuwa sababu ya stress zinazokukumba, mazingira yapo nayozungumzia mimi hapa? njia unayotumia kwenda kazini au kurudi nyumbani ina foleni sana? hiyo nayo inawea kuwa sababu ya stress ulizonazo, lakufanya epuka matumizi ya barabara kwa wakati huo, mazingira ya soko wakati wakufanya manunuzi ya bidhaa mbali mbali yanakupa stress? nenda katika supermarket maana kwa kiasi flani kuna utulivu na hali ya hewa nzuri
 
4.Epuka Hasira za haraka:Kuna ya mambo yanayohusu dini,siasa au maisha yako binafsi huwa yanakupa msongo wa mawazo basi jitahidi kuepukana nayo katika mazungumzo yako ya kila siku kwasababu yatakupa hasira na kukufanya ukasirike na hili hupelekea kuwa na msongo wa mawazo, ukiingia sehemu ukakuta watu wanaongelea swala hilo epuka nao ili usiweze kuchangia na kujikuta unaingia katika mgogoro wa nafsi
 
5.Tengeneza orodha ya vitu anavyotaka kufanya kwa siku :Ukiamka asubuhi , mara nyingi unapaswa kujua mambo ambayo ni ya lazima kuyafanya kwa siku ambayo unaianza ili ikifika jioni usiwe na viporo, katika orodha yako tenganisha orodha hiyo kwa vitu vya lazima kufanya na vitu vya kawaida ambavyo hata usipovifanya hazitakuharibia ratiba yako. kujua kipi cha lazima ni moja ya njia kubwa ya kupunguza msongo wa mawazo.
 
Naomba niishie hapa kwa leo na niseme ukizingatia hayo machache unaweza kuepuka Stress kwa kiasi kikubwa.
© MAISHA MAGAZINE | Blogger Template by Enny Law