Thursday, March 9, 2017

UZAZI:Mambo ya kuzingatia iwapo unataka kushika mimba mwanamke au mwanamke wako ashike mimba



Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu asishike mimba.
Sababu hizo zinaweza zikawa zinamhusu mwanamke, mwanamume au wakati mwingine kutojulikana kabisa hali hiyo imesababishwa na nini.
Wataalamu wanasema kwamba kwa miaka 20 iliyopita matatizo yanayohusu kushindwa kuzaa yameongezeka kwa kiwango kikubwa na asilimia 25 ya watu wanaotaka kubeba mimba na kuzaa mtoto wanakabiliwa na tatizo hilo.
Ni kweli kuwa kwa kawaida watu wengi hubeba mimba na kujaaliwa mtoto pale tu wanapofanya tendo la ndoa. 
Lakini jambo hilo halitokeo kwa watu wote na ingawa kwa baadhi ya watu kila kitu huonekana kwenda sawa lakini pia hushindwa kubeba mimba. 
Utafiti unaonyesha kwamba katika kila familia au 'couples' 5 zinazojamiiana katika wakati muafaka wa ovulation ni moja tu ndio hufanikiwa kupata mtoto, huku karibu wanawake 9 kati ya 10 wakifanikiwa kushika mimba baada ya kujaribu kutafuta mtoto kwa mwaka mmoja mzima bila kuzuia mimba.
Hivyo basi nawaomba wale ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kufuata maelekezo ili waweze kushika mimba lakini hawakufanikiwa, wasife moyo kwani ipo siku jitihada zao hizo zitazaa matunda.
Mambo ya kuzingatia iwapo unataka kushika mimba…
• Kwanza kabisa ni kuhakikisha kuwa kabla ya yote unamuona dokta wako au unakwenda hospitalini na kufanyiwa vipimo ili kujua kama afya yako iko salama au la kwa ajili ya kushika mimba. Baadhi ya vipimo vinavyoshauriwa kufanywa ni pamoja na
1. General examination au uchunguzi wa jumla.
2. Kipimo cha kensa au Pap smear.
3. Kipimo cha magonjwa ya zinaa (STD) kama vile Chlamydia ambao wanaweza kuathiri uwezo wako wa kushika mimba.
4. Kipimo cha damu cha kuangalia kama una upungufu wa damu, Rh na kinga yako ya mwili dhidi ya ugonjwa wa Rubella.
5. Kipimo cha mkojo cha kuchunguza iwapo una ugonjwa wa kisukari,kwani ugonjwa wa kisukari huweza kumzuia mtu asishike mimba hata iwapo mzunguko wake wa mwezi uko sawa, anapata Ovulation na dhahiri anaonekana hana tatizo lolote.
6. Kama una paka nyumbani au unakula sana nyama nyekundu(red meat) pengine si vibaya pia kupima kipimo cha Toxoplasmosis infection,kuangalia kama unamaambukizi yanayosababishwa na vimelea vya Taxopasma Gondii ambayo huweza sababisha tatizo la kupata Ujauzito.
7. Kuyajua na kuzingatia baadhi ya mambo yanayoathiri kushika mimba ambayo ni pamoja na:-
• Ingawa unene unaweza kumzuia mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa zaidi ya kilo 50 huweza pia kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya kupindukia pia huathiri homoni mwiilini.
• Kuwa na fikra nyingi na msongo wa mawazo 'stress' huweza pia kauthairi uwezo wa mtu wa kushika mimba.
• Kutokula vizuri na kutopenda kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanamme baadhi ya virutubisho muhimu vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba (nitazungumzia vyakula vinavyosaidia kushika mimba baadaye)
• Sigara, marijuana na pombe ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba. Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara. Mwanamume pia anashauriwa kuacha kuvuta sigara kwani sigara huathiri kiwango cha mbegu za kiume za mwanamme.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomsaidia mwanamke kushika mimba:
• Anza kutumia vidonge vya Folic Acid, vidonge hivyo mbali ya faida nyinginezo humkinga mtoto atakayezaliwa na magonjwa ya ubongo. (Neural Tube Defect) kama vile Spinal Bifida na mengineyo. Dozi ni kwa uchache miligramu 0.4 za Folic acid kwa siku, miezi mitatu kabla ya kuanza hata kutafuta mtoto.
• Endelea tu na tendo la ndoa bila kuchoka au kukata tamaa, lakini ni bora nguvu zihifadhiwe kwa siku chache kabla ya Ovulation na siku kadhaa baada ya hapo ili mwanamume aweze kuboreshe na kuhifadhi mbegu zake kwa ajili ya siku hizo, Usikimbie chooni au bafuni baada tu ya kukutana kimwili na mwenzio. Kulala kwa dakika kadhaa baada ya tendo la ndoa huongeza uwezo wa mbegu ya kiume kuweza kuendelea kukutana na yai la kike na hivyo kuongeza uwezekano wa kubeba mimba.
• Jiepushe kunywa kahawa na binywaji vinginevyo venye caffeine. Waataalamu wanasema caffeine huweza kukuongezea matatizo ya kushindwa kushika mimba.
• Jiepushe na kutumia dawa za aina yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinazonunulika maduka ya dawa bila ulazima wa cheti cha daktari au Over-the-counter drugs inabidi zitumiwe baada ya kushauriana na daktari.
• Usitumie baadhi ya vitu vinavyoufanya uke uwe na hali itakayoua mbegu za kiume au kupunguza majimaji yake. Vitu hivi ni kama spray mbalimbali na tampons zinazotumiwa na wanawake ili kuufanya uke uwe na harufu nzuri. Mafuta ya aina mbalimbali na jeli kwa ajili ya kulainisha sehemu za siri, mafuta ya kula (vegetable oils) glycerin na mate. Vitu kama hivi kufanya Ph ya uke isiwe ya kawaida na huweza kuua mbegu ya kiume, kusababisha baadhi ya magonjwa ya wanawake au kupunguza majimaji ya ukeni ambayo yanatakiwa ili kusafirisha mbegu za kiume.
• Hakisha mwenzi wako hafanyi kazi au hawi katika mazingira yenye mada hatari ambazo hupunguza uwezo wa mbegu za kiume au kutungwa mimba. Kufanya kazi kwenye mazingira ya joto kali sana kama vile mwanaume wanaofanya kazi kwenye matanuri ya kupika mikate, viwanda vya mafuta na miale hatari baadhi ya wakati huwa na matatizo ya kutozaa. Hivyo kabla mwanamke hajaanza kujilaumu kwa nini hashiki mimba, mwanamme wake pia anapaswa kufanyiwa uchunguzi kamili kuhusiana na suala hilo. Pengine ni suala ambalo wengi hatulijui kwamba katika tiba iwapo mke na mume au mtu na mwenzi wake wana tatizo la kutopata mtoto, wawili hao kwa pamoja hupaswa hufanyiwa vipimo na wala sio mwanamke mwenyewe. Hivyo iwapo unashindwa kushika mimba, hakikisha pia mwenzi wako hana tatizo pia. Wanaume pia kama walivyo wanawake hukabiliwa na matatizo mengi tu yanayosababisha familia kukosa watoto. Matatizo kama vile upungufu wa mbegu za kiume, uchache wa mbegu, kutokuwa na kasi mbegu na mengineyo ni miongoni mwa matatizo kibao ambayo mwanamume anaweza kuwa nayo na kukosa mtoto. Hivyo tabia ya kuwatizama wanawake kwa jicho la lawama katika jamii na kuwanyooshe kidole pale mimba inaposhindikana kushika ni kinyume cha ukweli wa kitiba na uhalisia.
• Usichoke kufuata mzunguko wako wa Ovulation na kufanya tendo la ndoa katika wakati ambao mwili wako (ewe mwanamke) uko katika siku za kuweza kushika mimba.

UREMBO:Njia kumi za Asili 10 zinazotibu chunusi


Tokeo la picha la FACE PIMPLE



CHUNUSI
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni.
Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani bakteria.
Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris. Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni 17.
Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe (adolescents).
1. Magadi Soda:
Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge hicho sehemu iliyoathirika na chunusi.
Kwa muda wa dakika 15 hadi 20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa maji yasiyo ya moto. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapoona athari za chunusi zimepotea.
2. Matango:
Unaweza kutumia Tango kwa kuondoa chunusi na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.
Matango ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kisha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Acha likae kwa muda wa dakika 15 hadi 20 hivi, kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu hadi utakapopona.
3. Kitunguu Swaumu:
Unaweza kutumia kitunguu swaumu kuondoa chunusi. Matumizi ya Kitunguu swaumu huleta matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na hata kuuwa bakteria sababu kina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili ya kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili).
Twanga kitungu swaumu, au unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi huku ukishikilia kwa dakika 5 mpaka 10, na kisha safisha na maji baridi. Waweza kufanya hivyo asubuhi na jioni.
4. Mnanaa (Peppermint):
Unaweza kutumia majani ya Mnanaa kuondoa chunusi usoni. Majani ya mnanaa hutumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa.
Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.
5. Limao:
Kata limao na kisha kwa kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwenye maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha acha pakauke, unaweza kurudia rudia kila baada ya masaa kadhaa.
Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa (ya dukani), kwa sababu yanaweza kuwa yamewekwa kemikali zingine ili kuyahifadhi kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao halisi.
6. Asali:
Matumizi ya asali kutibu chunusi huwezesha ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.
7. Papai:
Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na upakae sehemu yenye chunusi, kisha liache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kujisafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.
8. Dawa Ya Meno:
Unaweza kushangaa, lakini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.
Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanya kazi vizuri.
Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au ngano iliyosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.
Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.

9. Poda:
Unaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na kuiacha mpaka asubuhi.
10. Mvuke:
Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo huku ukielekeza uso wako kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke kwa dakika 5 mpaka 10 hivi. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.
MHIMU: Kunywa maji ya kunywa kila siku glasi 8 mpaka 10, jishughulishe na mazoezi ya viungo na ujiweke msafi kila mara.
Njia hizi za Asili zinaweza kuchukuwa muda kidogo mpaka kuona matokeo ya kuridhisha.
Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali iliyo karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.

Kama makala hii imekusaidia COMMENT & share na wengine

Tuesday, March 7, 2017

MAISHA:Chimbuko la siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa leo,na jinsi inavyoazimishwa

Kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujalia uzima mpaka kufika  na kuiona siku hii ya leo.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, tunayo adhimisha tarehe 8 Machi ya kila mwaka. Kwa mwaka huu kama ilivyo kawaida yetu Watanzania tunaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku hii Jumatano tarehe 8 Machi, 2017.
CHIMBUKO LA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Vuguvugu la Siku ya Wanawake lilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kupitia kwa wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa  wanawake.
  
Hatimaye Umoja wa Mataifa ulipoanzishwa mwaka 1945; tarehe 8 Machi iliridhiwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa pekee.
MADHUMUNI YA MAADHIMISHO

Madhumuni ya kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za Kimataifa/ kikanda  na kitaifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na wanawake katika kuhakikisha haki za wanawake kiuchumi, kijamii, na kisiasa zinapatikana na zinalidwa. 

Aidha, madhumuni mahususi ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango mkubwa wa wanawake katika kuleta maendeleo, kuelezea jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali na wadau wengine katika kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii ili waweze kushiriki kikamilifu kujiletea maendeleo yao, familia zao na Taifa kwa ujumla.
UTARATIBU WA MAADHIMISHO

Tanzania ilianza kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka 1996, maadhimisho yamekuwa yakiandaliwa Kitaifa na katika ngazi ya mkoa.

 Aidha, nikumbushe kwamba katika maadhimisho ya mwaka 2005 Serikali iliweka utaratibu wa kuandaa Maadhimisho ya Kitaifa kila baada ya miaka minne; ili kutoa fursa maalum kwa mikoa, wilaya na wadau wengine kupima mafanikio yaliyofikiwa katika kumwendeleza mwanamke katika ngazi hizo kwa miaka hiyo na ifikapo mwaka wa tano maadhimisho yafanyike kitaifa kwa kutoa taarifa ya utekelezaji kwa nchi nzima.

Mwaka huu kwa Dar es salaam mkuu wa mkoa huo,Paul Makonda ndiye  mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika , katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke Jijini Dar es Salaam,ila anawakilishwa na mkuu wa wilaya ya Temeke

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na  kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi”

Kauli mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa Wanawake  hasa kutambua mchango wao  katika kuleta Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.
Taarifa hiyo pia imeikumbusha jamii kuhusu wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa Wanawake haki sawa katika nafasi za Elimu, Uchumi na uongozi ili wawe chachu ya mabadiliko yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

MWISHO niseme hongera Wanawake wote dunia kwa siku hii muhimu ....wasalaam

UREMBO:Jinsi ya kupunguza unene haraka



tumbo


Uzito mkubwa wa kupindukia ni tatizo kubwa la kiafya katika maisha yetu ya kisasa. Uzito unapozidi kiwango ambacho kinahitajika kwa mtu husika kunachangia matatizo mengi ya kiafya. Watu wenye uzito mkubwa wamekuwa wakijaribu njia nyingi tofauti za kupunguza uzito bila ya mafanikio aidha kwasababu ya kukata tamaa mapema kabla ya matokeo au kwa kufuata njia zisizo sahihi na namna zisizo sahihi.
Baadhi ya matatizo yanayosababishwa na uzito mkubwa ni Kisukari ,Shinikizo la Juu la Damu na magonjwa mengine ya moyo.

Sababu za Kuongezeka Uzito wa Mwili:

Uzito mkubwa wa kupita kiasi unatokana na kuongezeka kwa mafuta mwilini ambayo hutunzwa sehemu mbalimbali mwilini kama juu ya ngozi,tumboni na juu ya viungo vya nadni vya miwili kama moyo,utumbo nk. Pia hujenga utando pembeni mwa mishipa ya damu.
Mafuta hutunzwa kama akiba pale mtu anapokula chakula kingi kuliko kiasi cha nguvu anazohitaji na hivyo mwili unabadilisha chakula hicho kuwa mafuta na kuweka katika akiba.
Watu wa mijini wananenepa zaidi kuliko wa vijijini kwasababu ya mitindo yetu ya maisha ambayo tunakula chakula kingi na chenye mafuta lakini hatuifanyishi miili yetu kazi za kutosha kutumia nguvu tulizoingiza.
Chukua mfano, mtu anakula kJ 5, mchana anakula kJ 20, jioni kJ 15 jumla ni Kj 40. Anaenda kazini kwa gari,anakaa masaa 8 kwenye kiti kazini kisha jioni anarudi na gari hadi nyumbani kwake. Umabali aliotembea ni mita 10-20 jumla ya nguvu ulizotumia jouli 30, nguvu zilizobaki bila matumizi ni kJ 10.
Sasa mwili unafanya nini na kJ 10 zilizobaki? Zinahifadhi kwa matumizi ya baadae kama mafuta ambayo hatakuja kuhitaji.
Fikiria inakuwaje katika siku 30 za mwezi na hifadhi hii. Hivi ndivyo uzito na unene unavyopatikana.
* kJ=Kilo Jouli (Kipimo cha nguvu mwilini)

Jinsi ya Kupunguza Uzito wa Mwili

  1. Kupunguza kiasi cha chakula kwa siku

kupunguza-uzito_ulaji-chakula
Hii ni njia moja kubwa ya kufanya usipate uzito mkubwa na pia kupunguza uzito.
Kama unahitaji kJ 30 kwa siku basi kama una uzito uliozidi utatakiwa kula kJ chache mfano kJ25 ili kJ 5 zinazohitajika zitoke katika akiba ya mafuta mwilini.
Uzito mkubwa unachangiwa kwa asilimia nyingi na kiasi kikubwa cha chakula mtu anachokula.
Naomba ifahamike kuwa suluhisho sio kuruka mlo,unatakiwa kula kila mlo ila kwa kiasi kidogo.
  1. Kufanya Mazoezi ya Mwili

kupunguza-uzito_mazoezi-2
Mazoezi ya mwili iwe kwa kufanya kazi au kwa kukimbia au katika vituo vya mazoezi au nyumbani yanasaidia kupunguza uzito kwa kuunguza mafuta ya akiba katika mwili. Mfano kama unakula kiasi unachohitaji tu kwa kazi za kawaida na kisha ukafanya mazoezi,mwili utahitaji kuchukua nguvu toka katika mafuta ili kujazia upungufu. Mfano unaweza ukatumia kj 10 kwa mazoezi ya dk 30 mpaka dk 60. Hivyo ukifanya mara kwa mara kama si kila siku utapungua tu uzito.
Mazoezi rahisi kufanya ni kukimbia kila jioni au asubuhi kwa umbali wa km 1 mpaka 2 zinatosha. Lakini unaweza kwenda katika kituo cha mazoezi jioni au ukanunua vifaa vya mazoezi na kufanya nyumbani kama unaweza.
  1. Mpango Sahihi wa Chakula-Chagua Kula Chakula Sahihi

kupunguza-uzito_chakula-1
Katika njia ya kwanza nimesema juu ya kiasi unachokula,hapa naelezea juu ya aina ya chakula unachotumia kinachangia uzito kuongezeka au vinginevyo.
Ulaji wa vyakula vingi vya wanga na mafuta ni chanzo kikubwa cha unene na uzito kuongezeka. Vyakula kama ugali,wali,mkate mweupe,bia na pombe za kienyeji zinazotokana na wanga (kimea) huchangia kuongezeka kwa uzito. Matumizi ya aina hii ya chakula ni muhimu kupunguzwa katika mlo wako.

Vitu vya kufanya katika mpango wa chakula:

  • Acha kula Vyakula vya Sukari

Sukari inayozidi mwilini toka katika vyakula hubadilishwa na kuwa mafuta. Vyakula kama chokuleti,biskuti,keki na vinyaji kama soda vina kiwango kikubwa cha sukari. Pia usitumie sukari nyingi katika chai na juisi.
  • Kula Mboga Mboga na Matunda Kwa Wingi

Mboga mboga ni nzuri kwa afya kwa ujumla lakini pia haina mafuta hivyo itakufanya kuingiza mafuta kidogo mwilini.
Matunda halikadharika hayapunguzi uzito moja kwa moja bali yatakufanya ushibe na usitamani kula kila mara kwani yanakata hamu ya chakula. Hivyo utaokoka na tabia ya kula kila mara ambayo huchangia sana kuongezeka uzito.
  • Acha Kula Kula Ovyo Nje ya Milo Maalumu

Uzito na kula kula hovyo ni marafiki wakubwa. Ukiona mtu ni mnene ujue anapenda kula. Ile kweli anakulakula ikimaanisha anakula kila mara na kila wakati chakula kinapokuwepo.
Anza leo kujenga tabia ya kula kidogo na katika milo muhimu mitatu.
  • Punguza Matumizi ya Chumvi

Ndiyo,chumvi inaongeza uzito. Sodiamu iliyomo katika chumvi inachangia katika mchakato wa kikemikali unaopelekea kuongezeka uzito. Tumia chumvi katika kiwango kidogo.
  • Tumia Chai ya Kijani

Umesikia kuhusu chai ya kijani (Green Tea), ni chai ambayo ni ya kijani na inasaidia kuondoa sumu za mwili (antioxadation). Hii inasaidia katika kusaidia mwili kuunguza mafuta katika njia inayoitwa thermogenesis.
  • Tumia Chai ya Tangawizi

Tangawizi kama ilivyo chai ya kijani inafahamika kuongeza mmeng’enyo wa chakula tumboni hivyo kupunguza mrundikano wa mafuta yasiyotumika
  • Kunywa Maji Mengi

Maji yanachangia kuharakisha mfumo wa uvunjaji chakula tumboni na hivyo kupunguza mafuta yanayohifadhiw

MAISHA:Hizi ndizo nchi 10 zenye wazee wengi zaidi duniani


Shirika la Afya Duniani ‘WHO’ limetoa orodha ya nchi zinazoongoza kwa watu wake kuwa na umri mkubwa zaidi duniani huku Japan ikitajwa kushika namba moja katika orodha hiyo ikifuatiwa na Italy. Kwa mujibu wa WHO karibu watu BILIONI 2 duniani wanatarajia kufikisha miaka 60 ifikapo 2050, ambapo itakuwa zaidi ya mara tatu ya ilivyokuwa mwaka 2000.
Japan inaongoza duniani ambapo 26.3% ya watu wake wana umri wa miaka 65 au zaidi ambapo mwaka 2014, ilikuwa ni 25.8%, ikimaanisha namba inaongezeka kila mwaka.
Top Ten ya nchi zenye wazee zaidi duniani

Namba Nchi % ya watu zaidi ya miaka 65
1 Japan 26.3 %
2 Italy 22.4 %
3 Greece 21.4 %
4 Germany 21.2 %
5 Portugal 20.8 %
6 Finland 20.5 %
7 Bulgaria 20.0 %
8 Sweden 19.9 %
9 Latvia 19.4 %
10 Malta 19.2 %
© MAISHA MAGAZINE | Blogger Template by Enny Law